CarolGK

MchangaNapenda lugha
Wafuasi
 1. Nchi nyingi Afrika kama vile Burundi na Tanzania ugonjwa wa Covid unaenea lakini serikali zao zimeamua kuzificha habari hizo. Tumeshuhudia miezi michache iliyopita vifo vya kutatanisha vya wakuu wa serikali za Burundi na Tanzania ambavyo hatuwezi dhibitisha kama kweli ni vya Corona au la, kwani seriSoma zaidi

  • 0
 2. Jibu hili limefanywa uhariri

  Nadhani nchi zitakazo ibuka mshindi kwa kupambana na virusi vya Corona Afrika mashariki ni Uganda na Rwanda. Hii ni sababu ya vikwazo vikali walivyoweka kuzuia maambukizi ya Corona. Pia wamesaidia wananchi wao kupata chakula na bidhaa zingine muhimu, wakati huu mgumu.  

  • 0
 3. Jibu hili limefanywa uhariri

  Kuzuiwa kutembea huru nchini ilifaa zaidi. Ukiangalia sasa hivi maambukizi na vifo vya Corona vimekuwa vingi zaidi vile watu wamekubaliwa tena kutembea huru. Wakati kulikuwa na vizuizi vya kutembea, maambukizi ya Corona na ata vifo havikuwa vingi sana kama sasa hivi.

  • 0
 4. Jibu hili limefanywa uhariri

  Mkutano ni mkutano ata ule wa kanisa ni mkutano. Ugonjwa hautambui haina ya mkutano na mikutano kama hii ndiyo inayochangia eneo la maambukizi ya Corona. Kwa hivyo ni vyema watu wakumbatie mfumo wa kidijitali wa kufuatilia mahubiri kwenye simu za rununu, redio ama televisheni. Pia watu wanaweza kwenSoma zaidi

  • 0
 5. Ndio, inafaa wasafiri wote wawekwe karantini siku kumi na nne kabla ya kuelekea makwao. Hasa sasa hivi safari za ndege za kimataifa zimerejelewa, ni bora zaidi kuwa makini. Nadhani kuzidishwa siku za karantini inatokana na ukosefu wa vifaa vya kutosha vya kupimia virusi ikilinganishwa na idadi kubwaSoma zaidi

  • 0
 6. Ndio. Afrika inafaa kukumbatia mfumo wa kusoma mitandaoni ila sio rahisi kwa ajili ya ukosefu wa vyombo vya teknolojia vinavyohitajika.

  • 0
 7. Jibu hili limefanywa uhariri

  Serikali inafaa kuondoa kodi kwa bidhaa zote za chakula na kuamuru bei ya chakula ipunguzwe kwa nusu ya bei. Hivyo hivyo wazilipe kampuni zinazotengeneza chakula hicho ili wasiende hasara.

  • 0
 8. Chakula ni ngumu sana kugawa inavyohitajika. Machifu wakipewa chakula kugawia watu watatumia njia ya mapendeleo kukigawa hicho chakula, kwa hivyo wengi watakosa. Hivyo, mimi naonelea ingekuwa bora zaidi serikali kutumia mfumo wa huduma namba kuzipata nambari za simu za watu wote wenye miaka kumi naSoma zaidi

  • 0
 9. Ndio, Walibora shujaa wa Kiswahili aliuliwa. Baada ya uchunguzi ilidhihirika kuwa Walibora alidungwa na kisu mara kadhaa kabla ya ajali hiyo. Ambacho hakijulikani kwa kweli ni nani alimuua na kwa nini. Cha kushangaza ni kuwa kuna ambulensi iliyopita hapo lakini haikumuokoa kwani hakuwa na pesa. MolaSoma zaidi

  • 0
 10. Jibu hili limefanywa uhariri

  Sababu inayofanya nchi za Afrika zisiendelee ni ufisadi na uongozi duni. Afrika ni bara lenye utajiri mwingi mno lakini utajiri huo umegawa kwa watu wachache sana ilihali kiwango  kikubwa cha watu kinabaki maskini na kikihangaika. Pili, waafrika wanaamini sana kusoma na kuajiriwa kuliko kutumia akilSoma zaidi

  • 0