Kideo

Rayvanny anaunga mkono na serikali ya Tanzania katika ngoma yake mpya ya Corona?

Nimefurahi kuona Rayvanny akitoa ngoma ya kuelimisha juu ya ugonjwa hasa kipande kile cha video kinachoonesha raisi wa Tanzania akieleza uzito wa corona. Mimi nataka kujua kama hii ndio wazo lake ama alishirikiana na mamlaka ya nchi? Iwapo hivyo mbona msanii mwengine hakuchaguliwa kama Diamond?

  1. Kwa vile kuna sauti ya raisi naona ndio ni mradi wa pamoja na serikali. Nchi nyingi wanatumia wasanii wao kusambaza tahadhari ya Corona. Hii ndio kingine cha africa.

    • 1
  2. Nadhani wasanii wengi sana Tanzania wanataka kujipendekeza kwa rais wao maghufuli. Hii ni kwa sababu si Rayvanny pekee ameonekana akitumia mbinu hii lakini pia Diamond na Harmonize hapo awali. Nadhani ni mbinu tu ya kujipendekeza kwa serikali ili waweze kuuza sera zao na kupata miradi kutoka kwa serikali.

    • 0
  3. Kuna hii ingine nilikutana nayo majuzi. Hiyo ni religious zaidi. Naona tusipoteze uamini na Mungu

    • 0

Inabidi kujilogisha kabla ya kuuliza swali