Ugonjwa wa Korona uliadhiri shughuli duniani kote. Nchi mingi zilizoadhirika zililazimika kusimamishwa shughuli zao za kawaida.
Siku chache zilizopita nchi mingi zimeonekana zikiwasihi raia wake kuendelea na shughuli zao za kawaida ili kuzuia kuzoroteka kwa uchumi?
Je, kwa maoni yako hatua hili linafaa kwa wakati huu?
Hatua ya Nchi mingi duniani kuamua kuendelea na shughuli zao za kawaida yafaa?
Shea
Ni vigumu kusema, lakini mvutano mkubwa ni kati ya maamuzi ya aidha kuendelea na shughuli huku zikichukuliwa tahadhari ama kusimamisha shughuli zote. Yote mawili ni maamuzi yanayofaa kwa kutegemea hali ya nchi husika na wananchi wake, hasa kiuchumu. Wakati nchi nyingi duniani zikiwa na changamoto nySoma zaidi
Ni vigumu kusema, lakini mvutano mkubwa ni kati ya maamuzi ya aidha kuendelea na shughuli huku zikichukuliwa tahadhari ama kusimamisha shughuli zote. Yote mawili ni maamuzi yanayofaa kwa kutegemea hali ya nchi husika na wananchi wake, hasa kiuchumu. Wakati nchi nyingi duniani zikiwa na changamoto nyingi za kiuchumi, ni vigumu kufunga shughuli zote. Je watu watakula nini? nchi itaendeshwaje? Wakati huo huo, kufunga shughuli na kungesaidia zaidi kuondokana na kirusi hicho kwa muda mpfupi iwapo hali za uchumi zingeruhusu kufanya hivyo.
Angalia kidogoNdio. Hatua hiyo inafaa kwa nchi ambazo tayari zimeweza kudhibiti virusi vya Corona na kumeonyesha kuwa hakuna mlipuko wa pili wa virusi hivyo. Lakini kwa nchi ambazo virusi bado havijadhibitiwa ama kuna mlipuko wa pili, sidhani ni jambo la busara. Wanafaa wavidhibiti kwanza na waweke mikakati ya kuSoma zaidi
Ndio. Hatua hiyo inafaa kwa nchi ambazo tayari zimeweza kudhibiti virusi vya Corona na kumeonyesha kuwa hakuna mlipuko wa pili wa virusi hivyo. Lakini kwa nchi ambazo virusi bado havijadhibitiwa ama kuna mlipuko wa pili, sidhani ni jambo la busara. Wanafaa wavidhibiti kwanza na waweke mikakati ya kuzuia mlipuko wa pili.
Angalia kidogo