Masharti ya Utumiaji

Ahadi Yetu

1. Kutoa Huduma Vizuri – Tutajaribu kutoa huduma vizuri lakini tunaomba subira wakati tunatayarisha tovuti yetu. Tutafanya kadiri tunavyoweza kuhakikisha kuwa maudhui ya kukera hayapo.

2. Kulinda Data Binafsi – Tatafanya bora yetu ya kulinda data zako ya binfasi. Hakikisha usiweke habari ya binafsi katika sehemu ya wasifa ilio wazi.

Haki Zetu

1. Kufuta Maudhui – Ikiwa tumeamua kuwa mtumiaji amekiuka sera zetu, tunaweza kufuta michango yake katika tovuti bila onyo. Kwa hatia nzito tunaweza kufuta akaunti na kuzuia usajili upya bila onyo.

2. Kuweka Maudhui Wazi – Tuna haki ya weka michango yako wazi tovutini (yakiwemo maudhui yote yaani mapicha, video, maandishi, na kadhalika). Kumbuka ya kwamba unavyoandika yatakuwa wazi. Bado unaweza kuomba kitu kifutwe.

3. Kukataa Matuzo – Tuna haki ya kukataa matuzo (yaani malipo madogo ya airtime) ikiwa tunashuku kuwa udanganyifu upo. La sivyo tutafanya bora yetu wanaopaswa kupewa matuzo watapewa.

Masharti ya Huduma

1. Toa ya Dhati – Humu tunaomba maandishi yenu yawe ya dhati na kamilifu kadiri iwezekanavyo. Vilevile msijifanye kuwa mtu ama shirika tofauti ya ukweli.

2. Heshimu Tovuti – Tumetia bidii ili kuandalia tovuti, kwa hivyo tunaomba isiharibike. Twambie ikiwa utapata shida yoyote katika tovuti yetu.

3. Fuata Sheria Husika – Tovuti yetu inapatikana kwa nchi nyingi. Kila nchi ina sheria yake kuhusu vyombo vya habari, vyombo vya jamii, hakimiliki, na kadhalika. Mnawajibika kwa maandishi yote mnayoweka tovutini.